Nature

Yanga; Hatuna Sababu ya Kuogopa Timu Yoyote Ligi ya Mabingwa

Baadhi ya mashabiki wa Yanga ni kama wameipokea ratiba ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa presha wakiona kama ni safari ngumu lakini uongozi wao umetoka hadharani na kutoa neno zito.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo, ameeleza kuwa ratiba hiyo wameipokea na sasa wanaanza hesabu za namna ya kukabiliana na mechi hizo sita.

“Unaweza kusema ni ratiba ngumu lakini sisi ni Yanga tunajua ubora wa wapinzani wetu lakini tutajipanga kukabiliana na timu moja kwenda nyingine bila unyonge.Tuna timu imara sana na hivi karibuni mmeona tumeboresha benchi letu la ufundi kwa kumleta kocha mkubwa, tuko kwenye afya nzuri ya kwenda kushindana.

“Tunakwenda kujipanga sawasawa, tutakutana na benchi la ufundi lakini yapo mambo yatakuwa hadharani na mambo mengine hayatakuwa wazi, sio kila taarifa ya kukabiliana na adui yako inatakiwa kufika kwa mpinzani.

“Mashabiki wetu hawatakiwi kutishwa, Yanga ni kubwa, wanaodhani tutaanguka, tunatakiwa kwenda kuwathibitishia kwa vitendo ukubwa wetu, kuna ratiba huko nyuma zilitoka tukaona tutashinda lakini tukakwama na kuna ratiba pia tuliziona ngumu baadaye tukatoboa.”

Related Posts