Klabu ya Young Africans SC Rasmi Imekuwa klabu ya kwanza kujiunga na Jumuiya ya Vilabu vya Afrika (ACA) jumuiya mpya iliyozinduliwa kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya soka la vilabu barani Afrika.
Mabingwa hao wa Tanzania wamekamilisha malipo yao ya ada ya uanachama yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,000 (zaidi ya Shilingi milioni 2 za Kitanzania) hatua inayowafanya kuwa miongoni mwa klabu waanzilishi wa mradi huu mkubwa wa bara.
Jumuiya ya Vilabu vya Afrika (African Clubs Association ACA) inaongozwa na Rais wa Yanga Hersi Ally Said ambaye amezihimiza klabu zote za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza barani Afrika kujiunga na jumuiya hiyo ili kwa pamoja kushiriki katika kujenga mustakabali mpya wa soka la vilabu Afrika.

