Nature

Yanga Kumchimbia Shimo Kocha Marcio Maximo Leo

JUMAPILI hii sio ya kukosa, Yanga baada ya kumaliza harakati za kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakuwa mwenyeji wa KMC, mechi ikipigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, kuanzia saa 10:00 jioni.

Mtego uliopo hapa ni wa aina mbili, Yanga dhidi ya KMC, mabingwa watetezi Yanga wanasaka ushindi utakaowasogeza nafasi za juu zaidi kutoka sasa ilipo, lakini Kocha Marcio Maximo anaweza kujichimbia shimo pale KMC akipoteza.

Katika mechi nane zilizopita, Yanga imeshinda zote dhidi ya KMC. Katika vichapo hivyo nane mfululizo, Yanga imefunga mabao 21, ikiruhusu moja pekee. Hali inayoonyesha KMC imekuwa Mteja mzuri wa Yanga.

KMC timu ambayo ushindi wao wa kwanza dhidi ya Dodoma Jiji, unabaki kuwa wa kukumbukwa zaidi kwani baada ya hapo, imeambulia vichapo vinne mfululizo, hali inayomweka matatani Kocha Marcio Maximo. Si katika ulinzi pekee, bali hata ushambuliaji KMC kuna tatizo, mechi tano imefunga bao moja la Rashid Chambo, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara sita. Yanga katika mechi tatu, imefunga mabao matano, haijaruhusu.

Related Posts