Yanga Mbioni Kunyan’ganywa Pointi Kisa Usajili Wenye Utata wa Damaro

Yanga Mbioni Kunyan'ganywa Pointi Kisa Usajili Wenye Utata wa Damaro
Yanga Mbioni Kunyan’ganywa Pointi Kisa Usajili Wenye Utata wa Damaro

Kuna kesi ipo pale TFF ya Simba SC dhidi ya mchezaji Mohamed Damaro na Yanga SC kuhusiana na uhalali wa mchezaji huyu kusajiliwa kama Mtanzania kwenye ligi yetu ilihali kwenye system za FIFA anasomeka ni raia wa Guinea 🇬🇳.

Yani Damaro akiwa Singida BS alisajiliwa kama raia wa Guinea, baada ya kubadili uraia na kupata passport ya Tanzania Yanga wakamsajili kama Mtazania na kuanza kumtumia bila kumuombea kibali cha kubadili Shirikisho/Chama cha Soka kama taratibu za FIFA zinavyosema ambapo FA (hapa Tanazania TFF) inawajibika kuwasilisha maombi FIFA (Kwa Katibu Mkuu) kwa niaba ya klabu na mchezaji HAPASWI KUTUMIKA mpaka apate kibali cha kubadili “uraia wa mpira” kutoka FIFA, kupitia Players’ Status Committee (PSC) kitu ambacho Yanga SC na Damaro HAWAJAFANYA kupitia TFF na mchezaji anatumika kwenye ligi na mashindano ya kimataifa KINYUME na taratibu kwa madai ya Simba SC.

Hali ilivyo ni kwamba kwenye mifumo ya TFF Damaro anasomeka kama Mtanzania lakini kwenye mifumo ya FIFA Mohamedi Damaro Camara anasomeka kama Raia wa Guinea 🇬🇳 akiwakilisha Shirikisho la Guinea – FEGUIFOOT na sio TFF, kwa mujibu wa Simba SC haipaswi kuwa hivyo, ipo hivyo kwa sababu taratibu hazijafuatwa ambacho ni makosa.

Hivyo Simba SC hawana shida na Damaro kuwa na passport ya Tanzania na kujulikana kama Mtanzania, wanaona uraia wa Damaro unamsaidia kwenye mambo mengine ya kisiasa na kijamii lakini sio kimpira, anaweza kupiga kura, kununua Ardhi kama Mtanzania, kuanzisha Kampuni, etc etc kama walivyo Watanzania wengine, lakini kwenye soka HANA UHALALI kwakuwa huku kuna taratibu za kufuata ili kubadilisha uwakilishi wa Shirikisho lako la zamani kwenda jipya ambao HAUJAFANYIKA na kwa mujibu wa wanasheria wa Simba SC haya na makosa na Yanga SC wanatumia wachezaji 13 wa kigeni kinyume na kanuni za Ligi Kuu, wameomba Yanga SC wapokwe alama zote katika michezo ambayo Damaro amehusika.

Unataka kuzifahamu taratibu za FIFA ambazo Yanga SC/Damaro kupitia TFF walipaswa kuzifuata, itaendelea NeXT Post …….. Don’t Miss.

BIN KAZUMARI MTIPA (The Real Voice of the voiceless)

Related Posts