Yanga Warahisishiwa Njia ya Kwenda Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika

Klabu ya Al Ahly SC imefungua rasmi mfumo wa mauzo ya tiketi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya AS FAR, huku mashabiki wakianza kununua tiketi kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka za usalama kuidhinisha idadi kubwa ya mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani, jambo linaloashiria kuwa mchezo huo utachezwa mbele ya umati mkubwa wa watazamaji.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Waziri wa Ulinzi Meja Jenerali Mahmoud Tawfik ameidhinisha jumla ya mashabiki 75,000 kuingia uwanjani. Idhini hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Al Ahly, na sasa imepitishwa rasmi baada ya Mkuu wa Usalama viwanjani kutoa ruhusa kamili.

Kwa idhini hiyo, Al Ahly wanatarajiwa kuwa na uwanja uliojaa kabisa, hali itakayoongeza hamasa na presha kwa wapinzani wao AS FAR. Hata hivyo, ni mashabiki 2,000 pekee kutoka AS FAR watakaoruhusiwa kuingia uwanjani, kulingana na taratibu za usalama zilizowekwa kwa mchezo huo mkubwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili hii katika uwanja wa Cairo International Stadium, na unatajwa kuwa miongoni mwa mechi zinazovuta hisia kubwa barani Afrika.

Mashabiki wa Al Ahly wanatarajiwa kuujaza uwanja huo na kuunda mazingira makali yatakayowapa nguvu wachezaji wao kuelekea ushindi.

Related Posts