Yanga Yaingia Vitani na Simba Kumgombania Mchezaji Luis Miquissone

Siku kadhaa baada ya Simba kufanya mawasiliano na Luis Miquissone sambamba na upande wa klabu yake inayommiliki (UD Songo) watani wao wa jadi, Yanga SC nao wametia maguu wakituma barua pepe kwenda klabu hiyo yenye makazi yake Msumbuji.

Taarifa za awali zinaeleza iwe Yanga wamejibiwa email kwa wakati ama vyovyote vile, kuonyesha uzito wa jambo lenyewe muda wowote rais wa klabu, Hersi Said atampandia ndege winga huyo hadi Msumbuji.

Ripoti ya kocha, Pedro moja ya mahitaji yake dirisha dogo ameahinisha hitaaji la kiungo mshambuliaji awe na sifa ya kucheza awe na sanaa ya kufunga, awe mwenye wastani mzuri wa kutengeneza nafasi, awe na kasi, nguvu, lakini pia awe mnyumbulifu kufungua pattern. Kiraka.

Inachokifanya Yanga ni muendelezo kwa nyota waliowahi kucheza Simba na baadaye wakaondoka, iwe ni mchezaji huru ama anakipiga timu nyingine wakati huo.

Fomu na takwimu za Miquissone zimekuwa kishawishi kikubwa kwa miamba hiyo ya soka nchini kila upande kutamani saini yake.

VITA IMEANZA🦁🔰

Related Posts