
KIGOMA: Kiongozi wa zamani wa #ACTWazalendo, ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho, #ZittoKabwe amejibu kauli za aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kuhusu ushirikiano kati ya ACT na CCM.
Amesema “Balozi huyo ni Mtu aliyechanganyikiwa na anahitaji kupewa dawa, amekuwa Mtu ambaye anaongea bila kutafakari.” Ambapo ameyasema hayo Agosti 27, 2025, mara baada ya kurejesha fomu ya kugombea Ubunge.

