Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Musa Azzan Zungu amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.
Zungu ameshinda kwa kupata kura 378 kati ya kura zote 383 zilizopigwa Bungeni wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu wa Bunge leo Novemba 11, 2025.

