
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ametoa tamko kwa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kufuatia uamuzi wa kushtua wa kuipokonya nchi yake taji la AFCON 2025 na kuwapa Morocco.
Katika kauli iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, Rais Faye amenukuliwa akisema: “Kama CAF haitabadilika na kuendelea kunyonya na kuingiza rushwa katika soka la Afrika, Senegal haitashiriki tena michuano yoyote ya CAF. Sisi si dhaifu wala waoga tena!”
