Gwiji Yaya Touré ametoa maoni yake kuhusu Fainali ya AFCON
“Mimi nimecheza mpira na kwa kweli nilikuwa sikubali kuonewa hasa mbele ya macho ya Dunia”
“Nimependa sana walichofanya Senegal , kuanzia benchi , wachezaji na kila mtu kwa kweli ilikuwa sahihi sana na hayo ni maoni yangu”
“Mimi sijali kuhusu Fairplay kama nanyimwa haki yangu , kama Senegal wasingefanya vile basi ndio ungekuwa mwisho wao na kombe wasingepata”
“Acha CAF na FIFA wawafungie viongozi na wachezaji hata kifungo cha maisha wala sio jambo la msingi , vipaji vipo na watakuja wengine mbeleni bora zaidi ila wameacha alama”
Gwiji Yaya Touré ameendelea kutoa maoni yake kuhusu Fainali ya AFCON
“Nimeona wakichukua taulo za magolikipa , unachukua taulo ya kipa wakati mvua inanyesha hii pia sio sawa , wamefanya hivyo dhidi ya Nigeria wamerudia tena kwa Mendy, wakiongelea fairplay tuulize Je kuchukua taulo za kipa huku mvua inanyesha hiyo ndio fair play !?”
“Morocco walijiandaa kufanya chochote ili wawe mabingwa , bahati nzuri Senegal walikuwa imara sana sio tu ndani ya uwanja bali hadi saikolojia “
“Siwezi kukubali kunyimwa haki kwa kisingizio cha Fair play, haitatokea milele , lile goli la Senegal lililokataliwa ni goli halali na kama wangefunga vile Morocco lingekubaliwa”
Mwisho.. Legend amemaliza hivyo
