TAKUKURU; Tunamtafuta Alex Msama Kwa Kuongoza Genge la Uhalifu, Zawadi Nono Kutolewa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwatafuta Alex Msama Mwita na Benny Mwita Sammoh kwa mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha kupitia Shauri la Uhujumu Uchumi Na. 1371/2026.

Naibu Mkuu wa #TAKUKURU Kinondoni, Elizabeth Mokiwa amesema jitihada za kuwapata hazijafanikiwa, hivyo yeyote mwenye taarifa zao aziwasilishe Ofisi yoyote ya TAKUKURU au kupiga simu Namba 0738 150236 na zawadi nono itatolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwao.

Amesema shauri la kwanza ni tuhuma za kughushi hati ya mauziano ya kiwanja kilichopo Vijibweni Kigamboni na kujipatia Tsh. Milioni 984 kati ya Tsh. Bilioni 1.7 iliyoainishwa kwenye mkataba wa mauzo. Pia, Msama anatuhumiwa kughushi na uvamizi katika eneo la kiwanja kilichopo Regent Estate Mikocheni. Hati za kuwakamata zilitolewa na Mahakama ya Kisutu, Januari 21 2026 na Shauri hilo litatajwa tena Februari 25, 2026.

Source; Jamii Forums

Related Posts