Morocco haitaandaa tena Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la 2030, kufuatia matukio wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Mashindano hayo ya 2030 yanatarajiwa kuandaliwa kwa pamoja kati ya Uhispania, Ureno, na Morocco, huku Morocco wakiwa katika kinyang’anyiro cha kuandaa mechi ya fainali.
Hata hivyo, mizozo kuhusu fainali ya AFCON kati ya wenyeji Morocco na Senegal imeripotiwa kuibua hali ya usalama na usimamizi ulio bora nchini humo.
Rafael Louzán, Rais wa Shirikisho la soka la Uhispania, alithibitisha kwamba Uhispania sasa itakuwa mwenyeji wa mechi ya fainali.
