Mwanamuziki Mkongwe wa nchini Marekani amejitabiria kutofika mwaka 2027 kwakuwa madaktari wamemwambia kuwa afya yake haiko sawa hivyo ni ngumu kufika 2027.Ray J ameweka hilo wazi kupitia akaunti za mitandao yake ya Kijamii huku akiwaacha mashabiki kwenye maswali mazito kwamba hizo taarifa ni za kweli au ameamua kutafuta kiki kama ilivyozoeleka kwa wasanii. Ray J anasema Moyo wake unashida hivyo ni ngumu kutoboa mwaka 2026
Wakati Ray J akitoa kauli hiyo anasikika rafiki yake aliyekuwa pembeni yake akimkataza kuwa na mawazo hayo kwani bado anakazi kubwa ya kuwale watoto wake na rafiki yake amesikika akimtia moyo.
Ray J ameweka kuwa anajutia jinsi alivyouharibu mwili wake kwa Pombe. Anasema alidhani mwili wake ungeweza kuhimili starehe zote lakini alikuwa anajidanganya. Ray J amewasihi vijana kutunza afya zao.
Ray J ni kati ya wasanii waliowahi kufanya vizuri duniani ambapo alitamba na vibao kamaOne Wish. Raydiation · 2005 · Sexy Can I (feat. Yung Berg). All I Feel (Bonus Track Version) · 2007 · Real Na Tendencies. Real Na Holiday.
