Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi , Aiomba Radhi Serikali ya Marekani

Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameiomba radhi Serikali ya Marekani, baada yeye, kuweka jumbe tata, kwenye Mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), ambazo baadaye alizifuta.

Katika jumbe hizo, Muhoozi alidai kuwa Ubalozi wa Marekani wa jijini Kampala, ulikuwa unahusishwa na siasa za upinzani nchini humo, na hata kutangaza kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Uganda na Marekani.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba, jana usiku alikuwa amezua taharuki kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutuma jumbe kadhaa za kuukosoa Ubalozi wa Marekani nchini Uganda kwa madai ya kumhifadhi Kiongozi wa Upinzani, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kwa jina la Bobi Wine.

Kyagulanyi alishika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu wa Januari 15, baada ya Rais Museveni, babake Jenerali Muhoozi, kutangazwa mshindi kwa kishindo.

Jenerali Muhoozi, ambaye pia ni mshauri mkuu wa Rais Museveni kuhusu operesheni maalum za kijeshi, alisema kwamba ubalozi wa sasa wa Marekani nchini Uganda ulisaidia sana Kyagulanyi kutoroka nyumbani kwake Magere, Wilaya ya Wakiso, katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika usiku wa Januari 16, 2026.

Related Posts