Kocha wa Al Ahly, Jess Thorup, amesema kuwa Yanga ni timu bora sana. Ameeleza kuwa hata katika mchezo wa kwanza walicheza vizuri na baadaye wakafanya mabadiliko ya kiufundi. Ameongeza kuwa wana wachezaji wengi wazuri mmoja mmoja, wenye uwezo mkubwa wa kushindana na kutoa upinzani mkali.
“Kuhusu Emam…! Hakukuwa na maelewano…! Alikosea na ameshaadhibiwa…! Hakuna mchezaji mkubwa kuliko Al Ahly na mtu yoyote ndani ya Al Ahly hawezi kuwa mkubwa kuliko Ahly…! Ameadhibiwa na anaweza kuadhibiwa zaidi sijui…! Kwa sasa tupo kwa ajili ya mchezo wa Yanga”
Jess Thorup Kocha wa Al Ahly
