CAF Kuchunguza na Kutathimini Pendekezo la FIFA Kuuza Hisa za Kombe la Dunia

CAF Kuchunguza na Kutathimini Pendekezo la FIFA Kuuza Hisa za Kombe la Dunia
CAF Kuchunguza na Kutathimini Pendekezo la FIFA Kuuza Hisa za Kombe la Dunia

Rais wa CAF Patrice Motsepe ataitisha Kamati ya Utendaji ya CAF wiki ijayo pamoja na mambo mengine, kuchunguza na kutathmini mpango unaopendekezwa wa FIFA.

Mpango wa FIFA unatarajia kuundwa na Kampuni FIFA Forward Enterprise (FFE) yenye jukumu la kusimamia, utangazaji wa shughuli zake za biashara na ufadhili wa tiketi.

Iwapo mradi huo utatekelezwa, kila nchi katika vyama 211 Wanachama wa FIFA inaweza kupokea bonasi ya Dola Milioni 20 mapema mwaka wa 2027 na mgao wake wa fedha kwa kipindi cha 2027–2030 ukiongezeka kutoka Dola Milioni 8 hadi Dola Milioni 20.

Hata hivyo, mradi huu uliotajwa Jumatano na Rais wa FIFA Gianni Infantino kama fursa ya dhahabu ya kuimarisha maendeleo ya mchezo huo duniani kote umeibua ukosoaji mkali, hasa kutoka kwa UEFA,mashirikisho makubwa ya soka barani Ulaya, na hata Umoja wa Ulaya.

Related Posts