Mangungu Afanyiwa Fujo Uwanja wa Taifa na Mashabiki wa Simba, Simba Watoa Tamko

TAARIFA KWA UMMA kutoka Simba

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kumvamia na kumfanyia fujo Mwenyekiti wa Klabu na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Murtaza Mangungu baada ya mchezo wetu dhidi ya ES Tunis kumalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Vitendo hivyo sivyo vya kiungwana, havikubaliki na havitafumbiwa macho. Uongozi wa Klabu unatoa pole kwa Mwenyekiti Mangungu kwa kadhia hiyo.

Aidha Uongozi wa Klabu umeliandikia Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika katika vurugu hizo au kula njama ili kuwafikisha katika Vyombo vya Sheria.

Bodi inasisitiza kuwa haitabariki wala kuvilia mtu yoyote atakayeharibu taswira ya Klabu kwa namna yoyote.

Related Posts