Alichokisema Mangungu Baada ya Kunusurika Kutembezewa Kichapo na Mashabiki wa Simba

Timu siyo yangu, kwanini kila siku mimi”, ni maneno yaliyosikika kutoka kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Sc Murtaza Mangungu mara baada ya kushambuliwa na kundi kubwa la mashabiki wa klabu hiyo dakika chache mara baada ya kumalizika kwa mechi ya CAFCL ambayo iliwakutanisha Simba Sc dhidi ya Esparance Sportive De Tunis.

Simba Sc walikuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao umepigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na umemalizika kwa sare ya kufungana 2_2.

Matokeo ya sare yamewaumiza mashabiki wa klabu ya Simba Sc ambao walijitokeza kushuhudia mchezo huo na baadhi yao kutokana na maamuzi yao ya hasira waliamua kumvamia mwenyekiti wao kwani wanaamini kwamba kiongozi huyo ndiyo chachu ya kuporomoka kwa ubora wa timu yao.

Mara baada ya jeshi la Polisi kuingilia kati na kumnusuru kiongozi huyo, Murtaza Mangungu amesikika akieleza wazi kwamba timu ya Simba Sc siyo ya kwake peke yake lakini wakati wote mambo yanapokuwa mabaya kwa maana ya timu inapopata matokeo mabaya lawama zote huwa anapewa yeye peke yake kitu ambacho kinamuumiza.

Murtaza Mangungu amewataka mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc watambue kwamba timu hii inaongozwa na viongozi wengine sana na yanapotokea mambo magumu basi viongozi wote wanapaswa kuwajibishwa kwa usawa tofauti na namna hii ambapo mashabiki wanamuandama yeye peke yake.

Mashabiki wa klabu ya Simba Sc wengi wao hawana imani na Murtaza Mangungu na pengine huu unaweza kuwa wakati sahihi wa kiongozi huyo kuachia ngazi ili nafasi yake ichukuliwe na kiongozi mwingine ambaye atakuja kuiongoza timu yao katika namna ambayo inaweza kupata mafanikio makubwa.

Related Posts