Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imesema imepokea kwa masikitiko makubwa vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo Dewji).
Bodi imeeleza kuwa uongozi wa klabu tayari umeiandikia Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wote waliohusika au waliokula njama katika mkutano huo, kwa lengo la kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Aidha, Bodi imesisitiza kuwa vitendo hivyo si vya kiungwana wala havikubaliki, na ikaeleza wazi kuwa haitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vinavyoharibu taswira ya klabu ya Simba SC kwa namna yoyote ile.
