Mangungu Noma na Nusu Awajibu Wanaotaka Ajiuzulu

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema hana mpango wa kuachia nafasi yake ya uongozi licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili klabu hiyo kwa sasa.

Mangungu ameeleza kuwa anaendelea kushika wadhifa huo kwa sababu wanachama na viongozi waliompa dhamana ya kuiongoza Simba bado wanamuamini na wanampa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.

Amesema akiwa kama kiongozi, anatambua uwepo wa changamoto ndani ya klabu, lakini ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Simba inazidi kupiga hatua na kurejesha mafanikio yaliyotarajiwa na mashabiki pamoja na wanachama wa klabu hiyo.

Aidha, Mangungu amesisitiza kuwa uongozi wake utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa klabu ili kuhakikisha malengo ya maendeleo ya Simba yanafikiwa, huku akiwataka mashabiki kuendelea kutoa ushirikiano na sapoti kwa timu yao.

Kauli ya mwenyekiti huyo inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na mijadala miongoni mwa mashabiki kuhusu mwenendo wa timu pamoja na uongozi wa klabu hiyo.

Related Posts