Yanga Yachapwa Moroccox Hesabu za Kufuzu Ngumu

MOROCCO; UNAWEZA ukakubali ni kweli mpira wa miguu huwa kuna wakati unaendana na bahati.

Pengine ndivyo unavyoweza kusema baada mchezo wa AS FAR Rabat ya Morocco na Yanga ya Tanzania kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika Uwanja wa Olimpiki nchini Morocco na kumalizika muda mfupi uliopita.

Kutokana na matokeo hayo Wamorocco wamefikisha pointi nane na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo na kuiacha Yanga ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi tano. Kundi hilo B linaoongozwa na Al Ahly yenye point inane pia.

Nafasi ya Yanga kufuzu robo fainali inatagemea matokeo ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya JS Kabylie, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ikitakiwa ishinde huku ikiombea AS FAR Rabat ipoteze kwa Al Ahly halafu Yanga ishindane na AS FAR Rabat uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa, maana wote watakuwa na pointi nane.

Mchezo wa leo Yanga walipambana kwa nguvu na walipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini walishindwa kuzitumia, kiasi kwamba kama nafasi hizo zingetumiwa vizuri, bila shaka matokeo yangekuwa tofauti.

Related Posts