
Patrick Vieira Atekuliwa Kuwa Kocha Mkuu Mpya wa Senegal
Shirikisho la Soka nchini Senegal limemtaza rasmi gwiji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Patrick Vieira, kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo (‘Lions of Teranga’).
Vieira, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998, anachukua mikoba ya Pape Thiaw aliyeachishwa kazi kufuatia Senegal kuondolewa katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026 nchini Marekani kwa kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Ubelgiji.
Akiwa na uzoefu mpana wa ukocha katika klabu kama New York City FC, OGC Nice, Crystal Palace, Strasbourg na Genoa, jukumu kubwa la Vieira litakuwa ni kuiongoza Senegal katika mechi za kufuzu na hatimaye kushiriki michuano ya AFCON 2027 itakayofanyika katika nchi za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda).
