Paul Makonda “Tumepokea CV Nyingi Lakini Tumeamua Kubaki na Gamondi”

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Tanzania imepokea CV nyingi za Makocha wengi walioonesha ya kutaka kuinoa Stars lakini Wizara ya Michezo na Mamlaka nyingine za Soka zimeona Kocha wa Stars, Miguel Gamond, aendelee na jukumu lake la kuifundisha Stars kwakuwa ni Kocha bora.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo February 09,2026, Makonda amesema “Tulipokea CV nyingi sana za Makocha wengi lakini maamuzi ya Serikali ni kwamba tubaki na Kocha yule ambaye ameshaanza, amewajua Wachezaji na wao wamemfahamu, Gamond amepewa Timu katika muda mfupi sana, ukitaka kujua Kocha mzuri unaangalia kipindi cha sub pamoja na kufanya analysis ya video za Timu anayokutana nayo lakini wakati wa kwenda uwanjani anapanga timu akiona Wachezaji wamebadilisha mchezo utaona improvement yake kila akifanya mabadiliko kipindi cha pili timu inakuja ikiwa na nguvu zaidi”

“Huo ndio uwezo wa Mwalimu tunaoutaka ambaye anaweza kusoma game na akajua namna ya kucheza na Timu pinzani, Rais wetu ameshampa stahiki zote ambazo Rais yupo tayari kuzitoa kwa Kocha”

Related Posts