
Naweza kutofautiana na wengi ambao wameuweka mzani kuegemea upande wa Yanga kuwa watapata ushindi.
Mimi ninaamini Simba ana asilimia 51 dhidi ya 49 kwa upande wa Yanga kuweza kupata matokeo chanya kwenye hii mechi.
Nitakupa sababu moja ndogo ila kubwa sana kwenye jicho la kiufundi.
Unaweza kushinda mchezo wa Soka kwa uchezaji wa kitimu, kwa maana ya muundo wa timu, Idara ya Beki, Kiungo na Ushambuliaji kuweza kuelewana vizuri sana.[ Team chemistry ]
Pia unaweza kushinda mechi kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. ambao hao wachezaji muda wowote wanaweza kukudhuru hata kama timu yako ipo vizuri kiufundi
Na hapa ndipo naiona Kete itakayosukumwa na Simba kushinda au kupata sare Derby ya leo.
Namuogopa sana Libasa Gueye
Namuogopa sana Anicet Oura
Namuogopa sana Ino Loemba
Namuogopa zaidi Chama aliyeamka vizuri.
Hizo zote ni ‘X-Factors’ ambazo muda wowote zinaweza kukuinua kwenye kiti, huku ukishuhudia nderemo na vifijo kwenye kibendera cha kona.
Simba wanaweza kuwa na madhaifu yao mengi, ila wanao wachezaji ambao muda wowote wanaweza kukuharibia sherehe
Oura mzuri sana 1 vs 1
Gueye mzuri sana 1 vs 1
Loemba na jicho la pass pia movements zake za hatari
Chama na ule utulivu wake mithili ya Beyonce akiwa anaoga kwenye Jacuzzi.
Zanzibar leo kuna mechi, Hakutakua na mnyonge kihivyoo!
