
𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : NBC Premier League
SINGIDA BLACK STARS 0-3 YANGA SC
⚽️ 39” Dube
⚽️ 45+2” Okello (p)
⚽️ 58” Mudathir
Nafikiri Singida kuanza na Back 3 nyuma ilitoa msingi sahihi kwao kuanza kutengeneza mashambulizi kutokea nyuma + Pipino mbele yao anarahisisha Singida kutoka nyuma kwa usahihi … tatizo kilikuwa ni nini kwao ?
1: Wanakuwa na idadi ndogo ya wachezaji kwenye kiungo ( rahisi kwa Yanga kupora mipira na kutengeneza “ Turnovers “ ) ngumu kwao kufika eneo la mwisho kwa combination play .
2: Yanga walizuia vizuri nafasi eneo la ndani : hakuna nafasi baina ya kiungo na walinzi , hakuna nafasi nyuma ya walinzi wa Yanga maana yake Singida wanalazimika kushambulia nafasi eneo la pembeni zaidi ambapo mawinga wa Yanga walizuia vizuri nafasi nyuma yao hawakuacha 1 vs 1 dhidi ya washambuliaji wa Singida .
✍🏼 Yanga waliamua kuimaliza hii game kwa “ MOMENTS “ yaani pale wanapopora mipira wanafanya maamuzi ya haraka sana ( Pasia mpira kwenye nafasi , movements ya wachezaji wa mbele + bila mpira wanakuwa na muundo mzuri wa kuzuia )
✍🏼 Kipindi cha pili , Yanga walienda kusolid kile walicho kuanza kipindi cha kwanza ( muundo mzuri kwenye kuzuia + uhatari kwenye turnovers ) , Singida Bs bado walikosa ubora hasa eneo la mbele na ilikuwa shida kushinda mipambano yao .
NOTE :
1: Prince Dube magoli 6 na Assists 1 msimu huu 🔥
2: Ahmed Pipino game passing yake ni nzuri🙌 .
3: Duke Abuya mzuri sana kuzuia nafasi + mtulivu akiwa na mali mguuni .
4: Maxi Nzegeli utamkuta maeneo mengi kiwanjani ( Tank lake lina wese 🔋)
5: Andre Koffie ngumu sana kukabiliana nae ✅
FT : Singida BS 0-3 Yanga Sc
Kwenye msimamo Yanga wamefikiaha alama 32 huku mtani wao Simba SC akiwa na alama 24 na mechi moja mkononi.
Kelvin Rabson
