
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Mali, Tom Saintfiet, ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji Kamili ambao wataingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Urusi.
Katika orodha hiyo, mlinda mlango namba moja wa Klabu Young Africans S.C., Djigui Diarra, ameachwa nje kwenye kikosi cha Mali ambacho kinatarajiwa kujiandaa kwaajili ya maandalizi ya kuikabili Urusi kwenye mchezo huo wa kirafiki.
Mbali na Diarra, majina mengine makubwa yaliyokosekana kwenye kikosi hicho ni pamoja na Amadou Haidara, Mamadou Sangare, na Lassine Sinayoko, huku kukiwa na wachezaji wengine kadhaa waliokosa nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi hicho cha Mali .
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka katika Shirikisho la soka nchini humo, Malian Football Federation, sababu kuu za kukosekana kwa nyota hao ni pamoja na Baadhi ya nyota kusumbuliwa na majeraha huku wengine wakipumzishwa pamoja na masuala ya kifamilia.
Hata hivyo, kiungo wa shoka wa Klabu ya Al Ahly SC ya nchini Misri Aliou Dieng, nae mi miongoni mwa nyota muhimu waliojumuishwa kwenye kikosi hicho cha Mali kwaajili ya kuimarisha eneo hilo la kiungo wa ulinzi ambalo linaundwa na nyota wengine ikiwemo Amadou Haidara ambae si sehemu ya kikosi hicho kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Urusi.
Mbali na nyota pia Mlinda mlango wa kikosi cha Stade Malien, N’goro Traore ambae amekuwa na kiwango bora Sana kwenye michuano ya CAF champions League akiiongoza Klabu hiyo hadi hatua ya robo fainali msimu huu na kuondoshwa na kikosi cha Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika kusini .
