Hatimaye Sheikh Walid Akabidhi Ofisi

Hatimaye Sheikh Walid Akabidhi Ofisi
Hatimaye Sheikh Walid Akabidhi Ofisi

Aliyekuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Kawambwa, leo Julai 18, 2026 amefanya makabidhiano rasmi ya ofisi kwa Kaimu Sheikh wa Mkoa huo, Sheikh Abbas Ramadhan katika Ofisi za BAKWATA Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Sheikh Walid amesisitiza umuhimu wa Viongozi kujitathmini na kuzingatia maadili ya Uongozi, akimwabia Sheikh Abbas, “Jitambue, badilika na wacha mazoea.”

Pia amewaomba Viongozi na Watumishi aliokuwa akifanya nao kazi kwa kipindi cha miaka mitatu kumpa ushirikiano Kaimu Sheikh wa Mkoa, Sheikh Abbas Ramadhan ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Makabidhiano hayo yanafanyika siku chache baada ya Baraza la Ulamaa la BAKWATA ambalo Julai 14, 2026, lilimsimamisha Sheikh Walid kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mienendo inayokiuka misingi ya kiuongozi ya Baraza hilo.

Related Posts