Harmonize Amjibu Diamond ‘Acha Kulia na Arena’ Watanzania Wanahitaji Maendeleo – Video

Harmonize Amjibu Diamond ‘Acha Kulia na Arena’ Watanzania Wanahitaji Maendeleo – Video
Harmonize Amjibu Diamond ‘Acha Kulia na Arena’ Watanzania Wanahitaji Maendeleo – Video

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana kujibu kauli iliyotolewa na Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz, katika mahojiano yake kupitia Wasafi FM, licha ya Diamond kutomtaja moja kwa moja jina lake.

Kupitia Insta Stori yake, Harmonize ameandika ujumbe mrefu wenye ujumbe unaogusa masuala ya kijamii na vipaumbele vya taifa, ambapo amekumbusha kauli ya zamani ya Diamond aliowahi kuwahimiza Watanzania wafanye kazi badala ya kulalamika. Harmonize amesema kuwa sasa inaonekana ni muda wa msanii huyo mwenyewe kuonyesha mfano wa kile alichokuwa anakihimiza.

Katika ujumbe wake, Harmonize amesisitiza kuwa Watanzania wanahitaji zaidi maendeleo muhimu kama elimu, afya, miundombinu ya barabara, pamoja na kuboresha kilimo kupitia upatikanaji wa mbolea kwa wakulima. Aidha, ameongeza kuwa nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika huduma za kijamii na siyo mambo yanayoonekana kama burudani au maslahi binafsi ya watu wachache.

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz.
Kauli hiyo imeonekana na wengi kama jibu la moja kwa moja kwa mjadala unaoendelea, huku ikizidi kuongeza mvutano wa muda mrefu uliopo kati ya Harmonize na Diamond Platnumz, ambao ulianza tangu Harmonize alipoondoka katika lebo ya Wasafi na kuanza safari yake ya muziki binafsi.

Hadi sasa, Diamond Platnumz hajatoa kauli ya kujibu moja kwa moja ujumbe huo wa Harmonize, lakini mashabiki na wadau wa muziki wanaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mjadala huu unaoendelea kuchukua sura mpya kila siku.

Kupitia insta stori ya Harmonize ameandika haya “MIEZI 6 HAIJAISHA ULIKUWA UNAWAAMBIA WATANZANIA WOTE FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA MUDA WAKO WAKUFANYA KAZI UMEFIKA UNALALAMIKA ALENA ALENA ALENA WATANZANIA WANATAKA ELIMU AFYAAA BARABARA MIRADI YA MAENDELEO ZAIDI TUWE NA NDEGE ZAIDI HOSPITALI KILA SEHEMU..!! MBOLEA KWA WAKULIMA KIUJUMLA MAISHA BORAA… !!! USIJIFIKILIE WEWE NA KUNDI CHACHE LA WASANII, MANESI, WALIMU NAKADHALIKA…!!!! FANYA KAZI ULIPE KODI JENGO LA DPP & MISHAHARA YA STAF WAKO…!!! WANAOMBA SANA NA WANATUAMBIA KILA KITU SORRY…!!! MY BROTHER NICE STUDIO ANYWAY…!!! ALENA ITAANZA KUJENGWA MWEZI WA SABA KWA TETESI NILIZO NAZO ..!!! MIMI NA WEWE OSO HIZO NI SIASA ANAZIFANYA !!! KWETU TUMUONE AMEOMBA KITU CHA MAAANA SERIKALI HAITAKI LOL…!! MAJIBU WALIYO MPA HAO VIONGOZI TOFAUTI TOFAUTI MBONA HASEMI ??? WE ALL LOVE MUSIC LAKINI ALENA SIO KITU MUHIMU SANA CHA KUIFANYA SERIKALI IONEKANE SIO SIKIVU..!!!! MAWAZO HAYA IM SURE DALWESH MOMO KAYAPITISHA NA JENGO ZIMA LA WASAFILI…!!!!! GOOD FOR THE GAME BROSK HII NDIO SHIDA YA KUWA MFALME….!!!! ANYWAYS”

Related Posts