Kelvin Nashon Afunguka Maisha Mapya Msimbazi: “Sijajihisi Mgeni Kabisa, Ushindani ni Mkubwa!”

Kelvin Nashon Afunguka Maisha Mapya Msimbazi: "Sijajihisi Mgeni Kabisa, Ushindani ni Mkubwa!"
Kelvin Nashon Afunguka Maisha Mapya Msimbazi: “Sijajihisi Mgeni Kabisa, Ushindani ni Mkubwa!”

Kelvin Nashon Afunguka Maisha Mapya Msimbazi: “Sijajihisi Mgeni Kabisa, Ushindani ni Mkubwa!”

Kiungo mpya wa Simba SC, Kelvin Nashon, ameanza rasmi maisha yake ndani ya msimbazi kwa tabasamu na morali ya juu, huku akiweka wazi kuwa mapokezi mazuri kutoka kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi yamsaidia kuondoa presha ya kujiunga na miamba hiyo ya soka nchini.

Nashon, aliyejiunga na Msimbazi kuelekea msimu mpya wa 2026/27, ameeleza kuwa kwa sasa akili na nguvu zake zote zipo kwenye maandalizi ya msimu (pre-season) ili kuhakikisha anakuwa kwenye kiwango bora cha kuipigania timu.

Akizungumzia hali ya kambi na ushindani wa namba, kiungo huyo mkabaji alisema:

β€œNimefurahi sana kujiunga na Simba, na wala sijajihisi mgeni kwa sababu wamenipokea vizuri mno. Mbele yetu kuna mashindano magumu, hivyo kila mmoja yupo makini mazoezini. Ukipoteza umakini kidogo tu, unaweza kupoteza nafasi yako.”

Aidha, Nashon amekiri kuwa mazingira ya Simba SC yana tofauti kubwa na klabu yake ya zamani kutokana na kiu kubwa ya mataji na mafanikio iliyopo Msimbazi, jambo linalomfanya kila mchezaji kupambana bila kukata tamaa.

Related Posts