
Familia ya mwigizaji na gwiji wa sanaa za mapigano, Chuck Norris, imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kifo chake, zikieleza kuwa zimejaa upotoshaji unaotokana na matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI).
Kupitia taarifa yao ya umma, familia hiyo imesema kuwa machapisho na video mbalimbali zinazozunguka mitandaoni kuhusu afya, mazingira ya kifo na historia ya maisha yake ni za uongo na hazina ukweli wowote. Wameeleza kuwa baadhi ya taarifa hizo zimefikia hatua ya kubuni maelezo ya kitabibu na simulizi zisizo sahihi kuhusu familia yake.
Familia hiyo imewahimiza mashabiki na umma kwa ujumla kutopokea wala kusambaza taarifa zisizo na uthibitisho, wakisisitiza kuwa taarifa sahihi zinapaswa kupatikana kupitia vyanzo rasmi vya familia au wawakilishi wake.
Wameongeza kuwa ingawa taarifa kuhusu maisha binafsi na hali ya afya ya Norris zimekuwa zikishughulikiwa kwa uangalifu na faragha, wameendelea kutoa heshima kwa mashabiki wanaoendelea kumuenzi kupitia kazi zake na mchango wake katika
