VIDEO: Mwimbaji Upendo Nkone Amuomba Msamaha Martha Mwaipaja

Mwimbaji Upendo Nkone Amuomba Msamaha Martha Mwaipaja
VIDEO: Mwimbaji Upendo Nkone Amuomba Msamaha Martha Mwaipaja

VIDEO: Mwimbaji Upendo Nkone Amuomba Msamaha Martha Mwaipaja

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Upendo Nkone, amemuomba radhi Mwimbaji mwenzake Martha Mwaipaja kufuatia kauli aliyoitoa kwenye moja ya mahojiano, akidai kuwa aliwahi kutishiwa Maisha kupitia simu.

Sakata hilo limeibuka leo katika mitandao ya kijamii, baada ya Martha Mwaipaja kuchapisha video akimtaka Upendo Nkone kueleza kwa ushahidi wa kisheria ni lini na wapi aliwahi kumtishia Maisha, pamoja na madai ya kuwasiliana naye kwa simu. Kauli hiyo ya Martha imeonekana kumlazimisha Upendo Nkone kujitokeza hadharani na kuomba msamaha.

Akizungumza, Upendo Nkone amesema kuwa yeye ni Mkristo na anaamini katika msamaha, hivyo ameona ni vyema kuomba radhi kwa kauli aliyoitoa kwenye mahojiano aliyofanya na Lilian Mwasha.

Akizungumza na AyoTV, Nkone amesema “Kazi ya Shetani ni kugombanisha na kuchonganisha Watu. Inawezekana sikupaswa kulisema suala hili hadharani, nilipaswa kubaki nalo kimya. Lakini nilipohojiwa, nikajieleza, na sasa naona imeleta madhara.

Nipo hapa kumuomba msamaha Mwimbaji mwenzangu Martha Mwaipaja. Naomba anisamehe popote nilipomuumiza au kufanya jambo ambalo hakulipenda. Halikuwa lengo langu. Mungu hapendi mvutano, anapenda amani. Nilizungumza kama simulizi ya jambo lililopita, lakini kwa sasa nashusha moyo na kumuomba anisamehe.” Amesema Nkone.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by millardayo (@millardayo)

Related Posts