
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeonya kwamba meli zozote za kijeshi zinazopita kwenye Mlango wa bahari wa Hormuz zitakabiliwa na “jibu kali”.
Kauli hiyo imekuja baada ya Kamandi Kuu ya Marekani kusema meli mbili za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani zinavuka njia ya kimkakati ili kutegua mabomu ya maji yaliyotegwa na Iran.
Kamandi ya Jeshi la Wanamaji la IRGC ilisema ina mamlaka kamili ya kudhibiti mlango bahari wa Hormuz na itashughulikia “vikali” majaribio yoyote kama hayo ambayo yanatajwa na Marekani. Iliongeza kuwa ni meli za kiraia pekee ndizo zitaruhusiwa kupita, na hiyo pia chini ya masharti maalum.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, IRGC ilisema wazi kwamba ufikiaji wa mlango wa bahari hiyo utadhibitiwa vikali. Harakati za kijeshi kutoka Marekani hazitavumiliwa, wakati huo usafirishaji wa raia unaweza kuendelea chini ya masharti yaliyodhibitiwa.
Kulingana na ripoti, karibu meli 100 zilivuka Mlango-Bahari wa Hormuz katika mwezi uliopita chini ya makubaliano na mazungumzo kadhaa ya malipo ya ushuru kwa Iran.
Ingawa siku ya jana Mazungumzo ya Marekani na Iran hayakufika muafaka ripoti kutoka nchi zote zinasema mazungumzo yana nafasi ya kuendelea licha ya mkwamo wa jana.
