
UONGOZI wa Simba SC umemrejesha mshambuliaji wake raia wa Ghana, Jonathan Sowah, lakini kwa sharti kwamba afanye mazoezi na timu ya vijana ya klabu hiyo chini ya umri wa miaka 20 (Simba U20).
Sowah alisimamishwa mapema mwaka huu wakati timu ilipokuwa Dodoma ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Februari kabla ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Katika kipindi hicho, alirudishwa Dar es Salaam na tangu wakati huo hajacheza mechi yoyote ya ligi au mashindano.
Ally alieleza kuwa kamati hiyo imeamua Sowah afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya uangalizi wa karibu.
Kurudi kwake kwenye kikosi cha wakubwa kutategemea mwenendo wake na kama kamati itaridhika na maendeleo yake.
