Mbeya City yaachana na Mecky Maxime usiku


Dar es Salaam. Kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Yanga, leo Alhamisi, Juni 16, 2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kimehitimisha mkataba wa Kocha Mkuu wa Mbeya City, Mecky Maxime na klabu hiyo.
Saa chache tangu mechi hiyo ilipomalizika, uongozi wa Mbeya City umetangaza kufikia makubaliano ya kusitisha ajira ya Maxime na wasaidizi wake wawili.

“Klabu ya Mbeya City Fc imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba wa Kocha Mecky Maxime pamoja na wasaidizi wake ambao ni Kocha msaidizi Nizar Khalfa na Kocha wa utimamu wa mwili Francis Mkanula.

“Tunatambua na kuthamini jitihada walizofanya katika kuboresha utendaji wa timu yetu na tunamshukuru kwa mchango wake uliotukuka kwa kipindi chote

alichoongoza timu yetu.

“Tunamtakia Kocha Mecky Maxime na wasaidizi wake

kila la kheri,” imesema taarifa ya Mbeya City.

Kichapo cha mabao sita kutoka kwa Yanga kimeendelea kuiweka Mbeya City katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi zake 17 ilizokusanya katika mechi 19.

Timu inayomaliza katika nafasi hiyo, kikanuni mara baada ya ligi kumalizika, inacheza hatua ya mchujo kuwania nafasi ya kubaki Ligi Kuu.

Maxime anaachana na Mbeya City baada ya kuitumikia kwa miezi minne tu tangu alipojiunga nayo rasmi, Desemba 7, mwaka jana akichukua mikoba ya Malale Hamsini ambaye naye mkataba wake ulisitishwa.

Katika miezi hiyo minne aliyoiongoza Mbeya City, Maxime amesimamia benchi la ufundi la timu hiyo katika mechi tisa za Ligi Kuu ya NBC ambazo imeshinda mbili, kutoka sare tatu na kupoteza nne.

Pia ameiongoza Mbeya City katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho la CRDB ikipata ushindi katika mechi moja na kupoteza nyingine.

Related Posts