Simba Wahamia KMC Complex Kwa Mechi Za Nyumbani

Simba Wahamia KMC Complex Kwa Mechi Za Nyumbani
Simba Wahamia KMC Complex Kwa Mechi Za Nyumbani

Klabu ya Simba SC leo Mei 7, 2026 wametangaza kuhamishia mechi zao za nyumbani katika Uwanja wa KMC Complex kwa michezo ijayo, wakiachana kwa muda na matumizi ya Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ambao ulikuwa ukitumika hapo awali.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya matumizi ya viwanja yanayoendelea kushuhudiwa kwa baadhi ya timu zinazoshirikiLigi Kuu.

Hatua hiyo inatarajiwa kuleta hamasa mpya kwa mashabiki wa Simba, ambao sasa wataelekeza nguvu zao KMC Complex kwa ajili ya kuisapoti timu yao katika mechi za nyumbani. Wengi wanaamini mazingira hayo mapya yanaweza kuwa chachu ya kuongeza morali kwa wachezaji na kuimarisha ushindani wa timu katika ligi pamoja na michuano mingine wanayoshiriki.

Related Posts