Prof. Anna Tibaijuka “Nashauri Tundu Lissu Aachiwe, 4Rs Itumike”

Prof. Anna Tibaijuka "Nashauri Tundu Lissu Aachiwe, 4Rs Itumike"
Prof. Anna Tibaijuka “Nashauri Tundu Lissu Aachiwe, 4Rs Itumike”

Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutumia hekima iliyomwongoza kutangaza sera ya 4Rs kumwachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa sababu kesi haikamiliki.

Kupitia ukurasa wake wa X, leo Julai 13, 2026 amesema “Dkt. Samia Suluhu, Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki, hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili”

“Simulizi hizi za kutisha za Vyombo vya Habari vya Kimataifa zinaibua hisia kali hasa kwa Vijana, hata Wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda Vijiji vya ujamaa 1974 -1976, taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya Taifa letu na maslahi yake, athari ni kubwa”

“Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano, tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa, tutubu na kusali kuliombea Taifa letu kila Mtu kwa imani yake”

Related Posts