Rais Samia “Msitumie Jina Langu”

Rais Samia "Msitumie Jina Langu"
Rais Samia “Msitumie Jina Langu”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hajaridhia kuendelea kwa matumizi ya jina la Mama Samia katika miradi, taasisi na programu mbalimbali, akisisitiza kuwa tayari kuna matumizi ya kutosha ya jina hilo katika Sekta ya Sheria.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania uliofanyika Jijini Arusha.

Amesema pamoja na mapendekezo mbalimbali yaliyowasilishwa katika mkutano huo, hakubaliana na pendekezo la kutumia jina lake katika Kituo cha Umahiri cha Sheria (Centre of Excellence in Law) kinachotarajiwa kuanzishwa.

“Tayari katika Sekta ya Sheria tuna Mama Samia Legal, nadhani tubakie na moja, hiki Kituo cha Umahiri cha Sheria tumtafute Mwanasheria mahiri, tumpe jina lake, kila sekta sasa ni Mama Samia inatosha,”amesema Rais Samia

Related Posts