
BAKWATA Yawasimamisha Kazi Masheikh Watatu wa Mikoa, Yumo Sheikh Walid Kawambwa wa Dar
Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewasimamisha kazi masheikh watatu wa mikoa kupisha uchunguzi, baada ya kubainika kuwa mienendo yao inakwenda kinyume na misingi, maadili na taratibu za uongozi wa baraza hilo.
Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha dharura cha Baraza la Ulamaa kilichoongozwa na Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Ngeruko.
Masheikh Waliosimamishwa na Kaimu Wao:
-
Sheikh Walid Alhad Omar Kawambwa (Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam)
-
Kaimu aliyeteuliwa: Sheikh Abbas Ramadhani Abbasi (Mjumbe wa Baraza la Masheikh Dar es Salaam).
-
-
Sheikh Issa Nasor (Sheikh wa Mkoa wa Singida)
-
Kaimu aliyeteuliwa: Sheikh Issa Simba.
-
-
Sheikh Hassan Kiburwa (Sheikh wa Mkoa wa Kigoma)
-
Kaimu aliyeteuliwa: Sheikh Uwesu Kiumbe.
-
Sababu za Kusimamishwa Kazi
Ingawa BAKWATA haijaweka wazi kwa undani makosa yaliyofanywa na viongozi hao, Katibu Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga, amethibitisha kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kukiukwa kwa maadili ya uongozi.
Aliongeza kuwa kusimamishwa kwao ni kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa kina wa kinidhamu kabla ya maamuzi ya mwisho kufanyika.
