KIMEUMANA: Sheikh Walid na Wenzake Kuanza Kuchunguzwa

KIMEUMANA: Sheikh Walid na Wenzake Kuanza Kuchunguzwa
KIMEUMANA: Sheikh Walid na Wenzake Kuanza Kuchunguzwa

Baraza la Ulamaa Taifa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeunda Tume Maalum ya Wajumbe sita kwa ajili ya kuchunguza tuhuma mbalimbali zinazowakabili Masheikh watatu wa Mikoa waliosimamishwa hivi karibuni.

Uamuzi huo umetangazwa leo, Julai 21, 2026 na Katibu Mkuu wa Baraza la Ulamaa BAKWATA, Sheikh Hassan Saidi Chizenga kufuatia kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Makao Makuu ya BAKWATA chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ali.

Sheikh Chizenga amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa Julai 14, 2026 ambapo Viongozi hao walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Masheikh wanaochunguzwa ni Sheikh Walid Alhad Omar wa Mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Issa Nassor Issa wa Mkoa wa Singida na Sheikh Hassan Idi Kiburwa wa Mkoa wa Kigoma.

Related Posts