Elizabeth Makune Aibuka Miss Universe Tanzania 2026

Elizabeth Makune Aibuka Miss Universe Tanzania 2026
Elizabeth Makune Aibuka Miss Universe Tanzania 2026

Elizabeth Makune Aibuka Miss Universe Tanzania 2026

DAR ES SALAAM: Elizabeth Makune kutoka Mwanza ametangazwa kuwa mshindi wa Miss Universe Tanzania 2026, baada ya kuibuka kidedea katika fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika katika studio za Haddy Pro, Mbezi Beach Jogoo, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Septemba 21, 2026.

Makune, ambaye aliwakilisha Mkoa wa Mwanza, amejishindia zawadi ya Sh milioni 20 pamoja na taji la Miss Universe Tanzania 2026.

Elizabeth Makune kutoka Mwanza mshindi wa Miss Universe Tanzania 2026.
Katika nafasi ya tatu, Sandra Giovina kutoka Arusha ametangazwa kuwa mshindi wa tatu na kupokea zawadi ya Sh milioni 10.

Melinda Enok ameshika nafasi ya nne. Mbali na zawadi ya Sh milioni 5, Enok atapata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Humanity, yanayotarajiwa kufanyika Hong Kong.

Nafasi ya tano imekwenda kwa Mariam Cosmas kutoka Mwanza, ambaye amepokea zawadi ya Sh milioni 5. Cosmas pia ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss OURA.

Sita bora ya Miss Universe Tanzania 2026.
Katika tuzo nyingine zilizotolewa kwenye fainali hiyo, Merikai Wavi ametangazwa kuwa Miss Supranational Tanzania, akipokea zawadi ya Sh milioni 10.

Fainali hiyo imewakutanisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, huku washindani wakipambana katika hatua mbalimbali za mashindano kabla ya majina ya washindi kutangazwa.

Ushindi wa Elizabeth Makune unamuweka katika nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Miss Universe, huku washindi wengine wakipewa majukumu ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya urembo ya kimataifa.

Related Posts