
Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Meja Kunta amefariki dunia leo Julai 21, 2026 katika Hospitali ya Temeke, Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu, huku chanzo cha kifo kikitajwa kuwa matatizo ya presha na stroke.
Akizungumza na AyoTV kwa njia ya simu, Meneja wa Meja Kunta, Wasowiso amethibitisha msiba huo na kusema taratibu za mazishi zinaendelea.
“Mzee ametutoka, taarifa tulipata kutoka kwa madaktari baada ya kufika hospitali na Mzee alikuwa ana shida ya stroke na presha,”amesema Meneja huyo.
