
Mchezaji Sakho Atangaza Kurejea Simba
Aliyewahi kuwa mshambuliaji hatari wa Simba Pape Ousmane Sakho, ameibua gumzo na kuzidi kuzua maswali kwa mashabiki wa klabu hiyo .ya Msimbazi.
Sakho ameacha ujumbe kwenye ukurasa wa Simba SC kwenye Instagram akisema: “Nakuja punde ndugu zangu”.
Ujumbe huo umezua maswali kwa sababu ya Sakho kuwa katika wachezaji wanaozungumzwa na Simba kurejea katika dirisha dogo la usajili.
Kwa sasa Sakho hana timu baada ya kuachana na Raja Casablanca ya Morocco, na tayari amerejea nchini Senegal akisubiri hatua inayofuata kwenye safari yake ya soka.
