Pigo Kwa Infantino: FIFA Yafuta Rasmi Mpango wa Kuuza Hisa za Mashindano Yake

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amekumbana na wakati mgumu kisiasa baada ya mpango wake wa kuuza sehemu ya hisa za mashindano ya FIFA kufutwa rasmi kufuatia shinikizo na upinzani mkali kutoka kwa wadau wa soka duniani.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, FIFA imethibitisha kuondoa mezani pendekezo hilo lililokuwa linalenga kuanzisha kampuni mpya ya kibiashara na kuuza asilimia 20 ya hisa zake kwa wawekezaji binafsi ili kuongeza mapato ya Kombe la Dunia na mashindano mengine.

UEFA Yamwekea Mpaka Infantino:
Upinzani mkubwa ulitoka kwa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), ambalo lilitishia kususia shughuli zote za FIFA ikiwa mpango huo ungedumu.

Mchambuzi wa uchumi wa michezo kutoka Chuo cha Holy Cross (Marekani), Victor Matheson, ameeleza kuwa ingawa Infantino alikuwa kwenye nafasi imara kifedha kufuatia mafanikio ya Kombe la Dunia lililopita, kufeli kwa mpango huu kumetikisa sana ushawishi wake wa kiutawala ndani ya FIFA na kuonyesha nguvu kubwa waliyonayo wanachama katika kupinga maamuzi yasiyo na tija kwa mchezo huo.

Related Posts