
Hatimaye hii leo mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga raia wa Namibia Peter Shalulile atawasili nchini kwa ajili ya kujiunga rasmi na kikosi cha Yanga.
Mara baada ya kuwasili klabu itafanya tukio la kumtambulisha kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine wakigeni waliotambulishwa kwa tukio la utambulisho kuwa ‘Live’.
Shalulile anatarajia kuwasili majira ya saa 5:00 usiku kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar Es Salaam.
