
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Ally Mangungu, ameshangazwa na maamuzi ya kubatilishwa kwa mkutano alioufanya jana huku akiweka wazi kuwa kuna watu wananufaika Simba ikiyumba na huko nyuma kuna watu walishatengeneza nyaraka kuwa Sima imeuzwa.
“Aliyebatilisha Mkutano wa Jana amebatilisha kwa Maamuzi yake au Maamuzi ya Bodi ?, Bodi ilikaa lini kubatilisha Kikao ?
“Labda kuna watu wananufaika Simba ikiwa inayumba ndio maana wanapigania, kuna mambo mengi yamefanyika ambayo wanasimba hawayajui.
“Huko nyuma kuna watu walishatengeneza nyaraka kuwa Simba imeuzwa, itafika wakati tutawataja,” Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu.
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo, huku akifafanua kuhusu maelekezo ya Serikali, utaratibu wa mikutano ya dharura, na jinsi uteuzi wa viongozi wapya ulivyofanyika.
Kauli za Mwenyekiti Murtaza Mangungu
1. Kuhusu Halali ya Uongozi na Mabadiliko ya Klabu
-
Mangungu amesisitiza kuwa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa Simba SC aliyechaguliwa na wanachama.
-
Ameweka wazi kuwa mabadiliko yoyote ya klabu hufanywa na Wanachama wa Simba SC kulingana na matakwa na taratibu za kisheria zinazowalazimu kufanya mabadiliko hayo.
2. Barua ya Serikali na Mkutano wa Dharura
-
Alieleza kuwa alipokea barua rasmi kutoka Serikalini na kuwasilisha maelekezo hayo kwa wajumbe wote wa Bodi kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi.
-
Katika kutekeleza maelekezo hayo, alipanga kufanya Mkutano wa Dharura mnamo Agosti 2, 2026, lakini aliarifiwa kuwa tarehe hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya maandalizi ya Simba Marathon.
3. Hali ya Amani Ndani ya Klabu
-
Amewatoa hofu mashabiki kwa kueleza kuwa yeye ndiye kiongozi mkubwa wa klabu na hakuna jambo baya linaloendelea ndani ya Simba, licha ya kuwa amekuwa akitazamwa na wengi kama chanzo cha migogoro.
4. Uteuzi wa Viongozi Wapya na Mzee Amos Makalla
-
Kuhusu viongozi walioteuliwa, Mangungu alieleza kuwa mchakato huo ulikuwa wa mashauriano kati yake na mwekezaji Mohammed Dewji (MO), ambapo MO alipendekeza majina 4 na yeye (Mangungu) akapendekeza majina 3.
-
Kuhusu jina la Amos Makalla, Mangungu alibainisha kuwa jina hilo lilipendekezwa na MO Dewji.
-
Aliongeza kuwa suala la kama Makalla alishauriwa au hakushauriwa si jukumu lake, lakini Makalla anayo haki ya kukubali au kukataa nafasi hiyo kwa kuwa alikuwa bado hajakabidhiwa barua rasmi ya uteuzi.
