
Klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji, Allan Okello ‘Star Boy’ kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Young Africans SC ya Tanzania
Nyota huyo wa Kimataifa wa Uganda mwenye umri wa miaka 26 anatua klabuni hapo kwa ada ya uhamisho iliyotajwa kuwa Dola za Marekani milioni 1.2 (takribani Shilingi bilioni 3.1 za Kitanzania)
