Azam FC Yapata Ushindi wa Kwanza Wakiwa Pungufu, Aisha Manula Alamba Kadi Nyekundu

Azam FC Yapata Ushindi wa Kwanza Wakiwa Pungufu, Aisha Manula Alamba Kadi Nyekundu
Azam FC Yapata Ushindi wa Kwanza Wakiwa Pungufu, Aisha Manula Alamba Kadi Nyekundu

Azam FC iliyokuwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Aishi Manula kuoneshwa kadi nyekundu imechomoza na ushindi wa 2-1 dhidi ya Wakusanya Mapato, TRA United katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwa Wanalambalamba hao baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ufunguzi huku TRA United ikishindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya sare kwenye mchezo wa ufunguzi.

FT: Azam FC 2-1 TRA United
⚽ 08’ Iddi Nado
⚽ 34’ Abdul Sopu
⚽ 46’ Kamisoko
🟥 77’ Manula

Related Posts