
Dogo Janja Afunguka Historia ya Uhusiano na Ndoa Yake na Irene Uwoya
Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, ameweka wazi maelezo kuhusu uhusiano na ndoa yake ya zamani na nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya.
Ndoa hiyo, iliyofungwa pindi Dogo Janja akiwa na umri wa miaka 22, ilizua gumzo kubwa na kushangaza mashabiki kutokana na tofauti ya umri kati ya wawili hao. Ingawa waliishi kama wanandoa kufuatia kufungwa kwa ndoa ya Kiislamu, mahusiano hayo hayakudumu kwa muda mrefu kabla ya kuachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Kauli hiyo imekuja kutoa ufafanuzi kuhusu mjadala uliodumu kwa miaka mingi miongoni mwa mashabiki, waliokuwa wakihoji iwapo ndoa hiyo ilikuwa ya kweli au ya kutengeneza kwa ajili ya kiki.
