
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba Mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.
Akiwasilisha hoja zake leo Agosti 17, 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ile aliyoiita Prima facie case (kutokuwa na kesi ya kujibu).
Lissu ameieleza Mahakama kuwa kuwa Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka pekee yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.
Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na maamuzi ya Mahakama katika kesi kadhaa ikiwemo ya kesi ya Rambaklal Trambaklal Bhatt dhidi ya Jamhuri amesema zimetengeneza misingi ya kisheria juu ya kitu gani mahakama inatakiwa kufanya kuhusiana na hoja ya kutokuwa na kesi ya kujibu.
Sababu ziliaoainishwa na mahakama hizo ni kuwa ni utiifu wa Jamhuri ya Muungano, lazima kuwe na uthibitisho wa nia ya kufanya kitendo cha uhaini na hiyo nia lazima ithibitishwe kwa maandishi au matendo ya wazi.
Anaeleza kuwa suala la utiifu kwa Jamhuri ya Muungano halina mjadala na suala lenye shida ni je kulikuwa na nia ya dhati ya kufanya uhaini akieleza kuwa katika maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ambayo aliyatoa April 3, 2025 na pia kupitia ushahidi wa mashahidi 17 wa jamhuri hakuna sehemu alipoonyesha nia ya kuitisha serikali kwani hakuna sehemu ilipotamkwa.
Lissu anasema kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani ya mwaka 2023, Sheria ya Kanuni ya Adhabu na sheria zingine hazithibitishi kosa la uhaini analodaiwa kulifanya.
