Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala

Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala
Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala

Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa mikoa kwa kuteua na kuhamisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala.

Taarifa iliyotolewa Agosti 27, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Bakari S. Machumu, inaeleza mabadiliko hayo kama ifuatavyo:

Wakuu wa Mikoa

Wateule Kipya:

  • CP. Salum Rashid Hamduni – Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga)

  • Alexander Pastory Mnyeti – Mkuu wa Mkoa wa Geita

  • Stanslaus Haroon Nyongo – Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani

  • Jumanne Abdallah Sagini – Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Waliohamishwa Kituo cha Kazi:

  • Martine Reuben Shigela – Kutoka Geita kwenda Mkoa wa Manyara

  • Said Mohamed Mtanda – Kutoka Mwanza kwenda Mkoa wa Simiyu (anachukua nafasi ya Anamringu Macha aliyestaafu)

  • Abubakar Mussa Kunenge – Kutoka Pwani kwenda Mkoa wa Songwe (anachukua nafasi ya Jabiri Omari Makame aliyepangiwa majukumu mengine)

  • Beno Moris Malisa – Kutoka Mbeya kwenda Mkoa wa Tabora (anachukua nafasi ya Paul Matiko Chacha aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC – Idara ya Oganaizesheni, CCM)

  • Adam Kighoma Malima – Kutoka Morogoro kwenda Mkoa wa Lindi (anachukua nafasi ya Zainab Telack aliyestaafu)

  • Queen Cuthbert Sendiga – Kutoka Manyara kwenda Mkoa wa Morogoro

Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS)

Uteuzi Mpya:

  • Richard Marcellino Kayombo – Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani

Waliohamishwa Kituo cha Kazi:

  • Balandya Mayuganya Elikana – Kutoka Mwanza kwenda Mkoa wa Mbeya

  • Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga – Kutoka Singida kwenda Mkoa wa Mwanza

  • Pili Hassan Mnyema – Kutoka Pwani kwenda Mkoa wa Shinyanga

  • Rodricks Lazaro Mpogolo – Kutoka Mbeya kwenda Mkoa wa Singida

Tarehe ya uapishaji wa viongozi hao wateule itatangazwa rasmi na Ikulu baadaye.

Related Posts